Monday, April 20, 2015

RIBERY HATIHATI KUIVAA PORTO.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amesema kuna hatihati ya winga Franck Ribery kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo wa maruadiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto. Ribery amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja na Guardiola amesema kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuukosa mchezo wa marudiano utakaofanyika jijini Munich baada ya kuchapwa kwa mabao 3-1 na Porto katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Ureno wiki iliyopita. Akihojiwa Guardiola amesema hadhani kama Ribery ataweza kucheza na pamoja na kwamba atazungumza na madaktari wao lakini hadhani kama ataweza. Guardiola ana matumaini ya kubadili matokeo katika mchezo huo huku akiendelea kuwa na msusuru ya majeruhi kwa wachezaji wake muhimu akiwemo Arjen Robben, David Alaba, Javi Martinez na Medhi Benatia.

No comments:

Post a Comment