Tuesday, April 28, 2015

WAKALA WA DE BRUYNE ADAI NYOTA HUYO ANA THAMANI YA EURO MILIONI 60.

WAKALA wa kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bruyne amedai kuwa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mteja wake huyo lakini amesema anaweza kuwagharimu kitita cha euro milioni 50 hadi 60. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ameimarika na kuja kuwa mchezaji muhimu katika klabu hiyo toka alipojiunga nao akitokea Chelsea Januari mwaka jana. Katika kipindi cha karibuni De Bruyne amekuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa Manchester City na Bayern Munich lakini wakala wake Patric De Koster amesisitia PSG ndio wako katika nafasi nzuri ya kunyakuwa kiungo huyo. Akihojiwa De Koster amesema PSG in klabu inayovutia na anadhani itakuwa sahihi kea mteja huyo kuitumikia. Hata hivyo De Koster aliendelea kudai kuwa mchezaji kama De Bruyne ana thamani ya kati ya euro milioni 50 hadi 60 kea soko la sasa na klabu zinazodai kuwa ziko tayari kutoa euro milioni 30 haziko karibu na ukweli.

No comments:

Post a Comment