Tuesday, April 21, 2015

PROMOTA AWA BUBU KUHUSU TIKETI ZA PAMBANO LA MAYWEATHER NA PAQUIAO.

PROMOTA Bob Arum bado ameshindwa kutoa ufafanuzi wa kwanini hakuna tiketi za jumla kwa ajili ya pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Manny Paquiao litakalofanyika jijini Las Vegas Mei 2 mwaka huu. Ukumbi wa MGM Grand una uwezo wa kuingiza watazamaji 16,500 lakini ni tiketi 1,000 pekee zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mashabiki wa kawaida wanaotaka kushuhudia pambano hilo. Inaaminika kuwa mkataba na ukumbi huo bado haujasainiwa wakati tiketi pia haziko sokoni kwa ajili ya kumbi nyingine zenye uwezo wa kuandaa pambano hilo. Arum alisitisha mkutano na wanahabari jana kabla ya hajaanza kuulizwa maswali. Bei ya tiketi za pambano hilo tayari imeshatangazwa kuwa kiasi cha kati ya dola 1,500 kwa tiketi za kawaida huku zile maalumu zikiwa dola 7,500.


No comments:

Post a Comment