Tuesday, April 28, 2015

BEKI WA UBELGIJI AANGUKA NA KUZIRAI AKIWA MAZOEZINI.

MCHEZAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Gregory Mertens amelazwa hospitali baada ya kuanguka wakati wa mchezo wa wachezaji wa akiba katika klabu yake. Beki huyo wa timu ya Sporting Lokeren mwenye umri wa miaka 24 alipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka katika kipindi cha kwanza na baadae kukimbizwa hospitali. Taarifa za klabu hiyo zinadai kuwa hali ya mchezaji huyo in mbaya na amewekwa katika hali ya kutojitambua huku akisaidia kupumua kea mashine katika hospitali ya Genk. Klabu hiyo pia ilituma salamu za pole kea familia yake huku wakimuombea mchezaji kuvuka kikwazo hicho kigumu katika maisha yake. Wachezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois anayecheza Chelsea na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku wote walituma salamu zao pole kea mchezaji huyo kupitia ukurasa wa mitandao yao ya twitter.

No comments:

Post a Comment