Thursday, April 30, 2015

INZAGHI ADAI BADO HAJAKATA TAMAA.

MENEJA wa AC Milan, Filipo Inzaghi amesisitiza hataki kukata tamaa pamoja nay a kuzuka kwa mjadala kuhusiana na mustakabali wake. Milan ilitandikwa mabao 3-1 nyumbani na Genoa jana na kuendelea matokeo mabovu kea timu hiyo katika mechi nne zilizopita hivyo kuwafanya kubakia katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Serie A wakipitwa alama tano na mahasimu wao Inter Milan. Kumekuwa na tetesi kuwa Inzaghi atatimuliwa mwishoni mwa msimu huu huku kocha Primavera Christian Brocchi akiripotiwa kuchukua mikoba yake. Hata hivyo, Inzaghi amepuuza tetesi hizo na kuwataka wachezaji kumaliza msimu wakiwa imara kea ajili ya heshima ya timu hiyo kongwe. Akihojiwa Inzaghi aliwapongeza wapinzani wao na kuomba radhi mashabiki wachache waliojitokeza katika Uwanja wa San Siro na kuahidi kuwa ataendelea kupambana kuhakikisha timu hiyo inarejesha heshima yake.

No comments:

Post a Comment