Tuesday, April 21, 2015

IBRAHIMOVIC KUONGOZA JAHAZI LA PSG.

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kurejea katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona leo. Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 33 alikuwa nje akitumikia adhabu wakati PSG walipochapwa mabao 3-1 jijini Parislakini anatarajiwa kurejea katika mchezo wa leo sambamba na kiungo marco Verratti. Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta naye yuko fiti pamoja na kutolewa nje katika mchezo wa wiki iliyopita kutokana na majeruhi. Luis Suarez ambaye alifunga mabao mawili murua katika mchezo wa mkondo wa kwanza anatarajiwa kucheza akiwa sambamba na washambuliaji wengine Lionel Messi na Neymar. PSG ambao wanakutana kwa mara ya nne na Barcelona katika michuano hiyo msimu huu itamkosa beki wake mahiri Thiago Silva.

No comments:

Post a Comment