Tuesday, April 28, 2015

GOLIKIPA WA ZAMANI MAN UNITED KUHUKUMIWA BAADA YA KUKIRI KUMGONGA MWENDESHA BAISKELI.

GOLIKIPA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Mark Bosnich amekiri kosa la kuendesha hovyo baada ya kumgonga na kumuumiza mwendesha baiskeli kea gari lake jijini Sydney. Bosnich mwenye umri wa miaka 43 alikwenda katika mahakama wa mji huo kusikiliza kesi yake kuhusiana na tukio hilo lililotokea Mei 21 mwaka jana. Golikipa huyo wa kimataifa wa zamani wa Australia anatarajiwa kuhukumiwa Juni 9 mwaka huu baada ya kumalizika kesi yake. Taarifa ya polisi inadai kuwa Bosnich ambaye pia amewahi kuzidakia timu za Aston Villa na Chelsea alimgonga mwendesha baiskeli huyo kwa upande na kumfanya kuanguka. Mwendesha baiskeli huyo alikimbizwa hospitali akiwa na majeruhi madogo katika sehemu za mbavu na kiwiko.

No comments:

Post a Comment