Friday, June 26, 2015

UCHAGUZI BARCELONA MOTO.

KAMPENI za urais katika klabu ya Barcelona zimezidi kushika kasi baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo Jordi Majo kuwaonya wapiga kura kuwa mgombea mwenzake Josep Maria Bartomeu anaweza kuhukumiwa na kwenda jela. Bartomeu ambaye alichukua nafasi ya Sandro Rosell aliyejiuzulu Januari mwaka 2014, kwasasa anakabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi inayohusu uhamisho wa Neymar uliofanyika miaka miwili iliyopita. Kumekuwa na masuala kadhaa ya kisheria yanayomkabili Bartomeu ambayo yametajwa na Majo anayedhani mpinzani wake huyo hakuchukua hatua stahiki kukabiliana nayo. Kutokana na hayo, Majo anadhani si vyema kwa Bartomeu kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo kwani anaweza hata kwenda jela kama akikutwa na hatia. Uchaguzi rasmi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu, wiki nne kabla ya msimu ujao wa La Liga haujaanza ambapo Barcelona chini meneja Luis Enrique watakuwa wakitetea taji lao.

No comments:

Post a Comment