Friday, June 26, 2015

COPA AMERICA: PERU KUKWAANA NA WENYEJI CHILE NUSU FAINALI.

MABAO matatu yaliyofungwa na mshambuliaji Paulo Guerrero yalitosha kuipa Peru ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bolivia na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa America. Guerrero alifunga mabao mawili ndani ya dakika tatu katikati ya kipindi cha pili na kuipa Peru uongozi katika mchezo huo wa robo fainali uliofanyika huko Temuco. Peru ambao pia walitinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2011 sasa watakwaana na wenyeji Chile mchezo ambao utafanyika huko Santiago Jumatatu ijayo. Mechi zingine za robo fainali zitawakutanisha Argentina dhidi ya Colombia Jumamosi na Brazil dhidi ya Paraguay Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment