Monday, June 29, 2015

STUTTGART YASAJILI GOLIKIPA WA DORTMUND.

KLABU ya Stuttgart imefanikiwa kumsajili golikipa Mitchell Langerak kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka kwa mahasimu wao Bundesliga Borussia Dortmund. Nyota huyo wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Dortmund akitokea Melbourne Victory mwaka 2010 na kufanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza Februari mwaka uliofuata wakati Dortmund walipotandikwa mabao 3-1 na Bayern Munich. Msimu uliopita Langerak ambaye alikuwa golikipa namba mbili wa Dortmund alicheza mechi tisa za Bundesliga. Langerak amelazimika kuondoka baada ya meneja mpya wa Dortmund Thomas Tuchel kumleta Roman Burki kutoka klabu ya Freiburg mapema mwezi huu.

No comments:

Post a Comment