Monday, June 29, 2015

CLYNE KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA LIVERPOOL.

BEKI wa Southampton Nathaniel Clyne anatarajiwa kujiunga na Liverpool muda wowote wakati meneja Brendan Rodgers akiendelea kukisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, tayari amesharejea kutoka mapumzikoni na atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake ambao umegharimu kiasi cha paundi milioni 12.5. Kila kitu kikikamilika, Clyne atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Mipango pia imeshaandaliwa kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino bada ya kumaliza majukumu yake ya kimataifa kwa kutolewa katika michuano ya Copa America na Paraguay Jumamosi iliyopita. Wengine ambao tayari wameshaanguka saini zao mpaka sasa ni kiungo wa Manchester City james Milner, mshambuliaji wa Burnley Danny Ings na golikipa wa Bolton Wanderers Adam Bogdan.

No comments:

Post a Comment