Monday, June 29, 2015

LIGI YA MABINGWA AFRIKA: MAZEMBE YAVUTWA SHATI NA AL HILAL.

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC jana imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kung’ang’aniwa sare ya bila kufungana na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mchezo huo Mazembe walionyesha soka safi lakini walishindwa kuipenya ngome ya Al Hilal mbele ya mashabiki wao waliojazana katika Uwanja wa Kamalondo uliopo jijini Lubumbashi. Katika mchezo mwingine wa kundi A uliochezwa jana timu ya Smouha ya Misri walifanikiwa kuitandika Moghreb Athletic Tetouan ya Morocco kwa mabao 3-2. Sasa Tetouan ambao wanashiriki hatua hiyo kwa mara ya kwanza watavaana Mazembe katika mchezo wao utakaofanyika Julai 10 mwaka huu. Kwa upande wa Al Hilal wao wataivaa Smouha wikiendi hiyohiyo.

No comments:

Post a Comment