Monday, June 29, 2015

COPA AMERICA: JARA FUNGIWA MECHI TATU KWA KOSA LA "KUMNAWA" CAVANI.

BEKI wa timu ya taifa ya Chile, Gonzalo Jara anatarajiwa kukosa michezo inayoendelea ya Copa America baada ya kunyukwa adhabu ya kutocheza mechi tatu kwa kosa la kumshika makalio mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani. Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-Conmebol limedai kuwa wamefikia uamuzi kutokana na beki huyo kuonyesha tabia isiyokuwa ya kiuanamichezo. Mbali na adhabu hiyo lakini Jara ametundikwa faini ya dola 7,500. Tukio hilo lilitokea wakati Chile waliposhinda bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika Alhamisi iliyopita. Cavani alimtundika kibao Jara baada ya kufanyiwa kitendo hicho hatua ambayo ilipelekea mwamuzi kumlima kadi ya pili njano na hivyo kutolewa nje. Adhabu hiyo inamaanisha Jara ataukosa mchezo wa leo wa nusu fainali dhidi ya Peru pamoja na mechi nyingine ya aidha fainali au kutafuta mshindi wa tatu kutegemeana na matokeo watakayopata leo.

No comments:

Post a Comment