Friday, June 26, 2015

PETR CECH HUYOOO ARSENAL.

GOLIKIPA wa Chelsea Petr Cech anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal leo ili kukamilisha taratibu za mwisho za uhamisho wake Emirates. Klabu hizo mbili tayari wameonekana kufikia muafaka wa ada ya uhamisho huku Cech mwenye umri wa miaka 33 akiwa tayari ameshakubali mambo yake binafsi. Golikipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo majira haya ya kiangazi. Cech ameamua kuondoka Arsenal baada ya kunyang’anywa namba katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na golikipa wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois mwenye umri wa miaka 23. Cech ambaye ameichezea Chelsea zaidi ya mechi 300 katika kipindi cha miaka 11, alifanikiwa kushinda mataji manne ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la FA, matatu ya Kombe la Ligi, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la Europa League.

No comments:

Post a Comment