Tuesday, June 23, 2015

KINDA LA CHELSEA KUTOKA BURKINABE LAPATA KIBALI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burkina Faso, Bertrand Traore sasa anatarajiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea baada ya kupata kibali cha kazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 alisajiliwa na Chelsea Januari mwaka 2014 lakini alikuwa hajafuzu kupata kibali hivyo kumfanya kupelekwa kea mkopo katika klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi. Chelsea iliomba tena kibali kipindi hiki cha kiangazi na kufanikiwa kupata chini ya mfumo mpya wa Chama cha Soka cha Uingereza. Traore sasa anatarajiwa kuwepo katika ziara ya Chelsea watakayoifanyika nchini Marekani ambapo watacheza na timu za New York Red Bulls, Paris Saint-Germain na Barcelona kama sehemu ya maandalizi kea ajili ya msimu ujao.


No comments:

Post a Comment