Tuesday, June 23, 2015

MANDZUKIC AMWAGA WINO WA MIAKA MINNE JUVENTUS.

KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia, Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid kwa ada ya paundi Milioni 13.6. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekamilisha vipimo vya afya jana jijini Turin kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Italia. Mandzukic anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Juventus kuelekea msimu mpya, baada ya awali kusajiliwa mshambuliaji wa Argentina, Paulo Dybala kutoka Palermo na Sami Khedira kutoka Real Madrid mapema mwezi huu. Akihojiwa Mandzukic amesema anafuraha kubwa kutua katika klabu kubwa kama Juventus na ana matumaini makubwa ya kuisaidia timu hiyo kushinda mataji zaidi.

No comments:

Post a Comment