Tuesday, June 30, 2015

WOLFSBURG YADAI HAWANA MPANGO WA KUMUUZA DE BRUYNE.

MKURUGENZI wa michezo wa Wolfsburg, Klaus Allofs amesisitiza kuwa klabu hiyo haina mpango wowote wa kumuuza Kevin De Bruyne katika usajili wa majira haya ya kiangazi. Manchester City ndio wanaoenekana kumuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji huku mwenyewe akithibitisha amepama mwezi huu kuwa wakala ameshafanya mazungumzo na klabu hiyo. Hata hivyo, Wolfsburg bado wameendelea na msimamo wao wa kutotaka kumuacha De Bruyne na Allofs amebainisha kuwa klabu hiyo inatarajia kuangalia uwezekano wa kumboreshea maslahi katika mkataba wake nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. Allofs amesema De Bruyne ana mkataba na Wolfsburg unaomalizika mwaka 2019 na tayari wameshatuma ujumbe kuwa hawana mpango wa kumuuza. Mkurugenzi huyo aliendelea kudai kuwa kikubwa wanachotizama hivi sasa ni kupitia upya mkataba wake na kuangalia jinsi ya kuuboresha zaidi.

No comments:

Post a Comment