Tuesday, June 30, 2015

HIDDINK AACHIA NGAZI UHOLANZI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink ametangaza kuachia nafasi hiyo kufuatia kusuasua kwa kikosi cha nchi hiyo katika michuano ya kufuzu michuano ya Ulaya mwakani. Katika taarifa yake Shirikisho la Soka nchi hiyo-KNVB ilithibitisha taarifa hizo huku mkurugenzi wake Bert van Oostveen akidai kuwa pamoja na kuwa kazi ya kocha huyo ilikuwa bado haijaonekana machoni kwa wengi lakini anashukuru kwa muda wote waliokuwa naye. Hiddink ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika baada ya michuano Ulaya mwaka 2016 amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kuinoa timu hiyo kwa mara ya pili na kuongeza kuwa anamtakia kila la heri kocha atakayechukua nafasi yake. KNVB kwasasa itakutana kuangalia jinsi ya kuziba nafasi hiyo huku msaidizi wa Hiddink, Danny Blind alitajwa kuwa ndiye atakayechukua nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment