Thursday, June 25, 2015

BOCA JUNIORS YATHIBITISHA KUAFIKIANA NA JUVENTUS KUHUSU TEVEZ.

KLABU ya Boca Juniors imetangaza kuwa Carlos Tevez anatarajiwa kurejea katika timu hiyo ambayo ndio aliyoanza kucheza soka lake baada ya kufikiwa makubaliano na mabingwa wa Italia Juventus. Katibu Mkuu wa Boca, Cesar Martucci alikaririwa na redio moja nchini Argentina akidai kuwa usajili wa Tevez umeshakamilika, ingawa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka Buenos Aires au Turin. Martucci amesema wana furaha kubwa baada ya kufanya kazi kubwa hatimaye wameweza kumshawishi Tevez kurejea tena nyumbani. Ingawa Martucci hakutoa taarifa za ndani zaidi kuhusiana na dili hilo lakini amesema Tevez anatarajiwa kutambulishwa mbele ya mashabiki wa Boca katika Uwanja wa Bombonera Julai 7 mwaka huu. Tevez mwenye umri wa miaka 31, aliwahi kuichezea Boca kuanzia mwaka 2001 mpaka 2004 kabla ya kutimkia Corinthians ya Brazil na baadae kutimkia Ligi Kuu katika klabu ya West Ham United mwaka 2006. Nyota huyo baadae alihamia Manchester United kabla ya kuhamia kea majirani zao Manchester City kea kitita cha paundi milioni 40 mwaka 2009 na kukaa hapo kwa misimu kisha kwenda Juventus mwaka 2013 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment