Thursday, June 25, 2015

BRAZIL BADO HAWAJASAHAU KIPIGO CHA UJERUMANI - TAFFAREL.

GOLIKIPA wa zamani wa Brazil, Claudio Taffarel anaamini kovu la kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana bado lipo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Paraguay. Brazil imefanikiwa kushinda mechi 12 kati ya 13 walizocheza toka wamalize katika nafasi ya nne katika Kombe la Dunia ambapo walishuhudia wakitandikwa mabao 10 katika mechi mbili kikiwepo kipigo cha mabao 7-1 kutoka kea Ujerumani katika mchezo nusu fainali. Pamoja na ujio wa kocha mpya Dunga kubadilisha mwelekeo wa kikosi hicho, Taffarel amedai wachezaji bado hawajapona sawasawa aibu waliyoipata kutoka katika michuano hiyo. Taffarel amesema itachukua muda wachezaji hao kusahau kipigo hicho lakini anaamini itafikia wakati watarejesha hali yao ya kujiamini na kuwaletea tena furaha mashabiki wa soka nchini Brazil na duniani kea ujumla.

No comments:

Post a Comment