Thursday, June 25, 2015

TABAREZ AMTETEA CAVANI BAADA YA BEKI LA CHILE 'KUMNAWA'.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez amemkingia kifua Edinsoni Cavani aliyetolewa nje jana katika mchezo war obo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya wenyeji Chile. Katika mchezo huo Uruguay walivuliwa ubingwa na wenyeji hao kea kufungwa bao 1-0 huku Cavani akionekana kuchangia bao hilo kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kea kumpiga kibao beki wa Chile Gonzalo Jara. Picha za video zinaonyesha kabla ya Cavani kutenda kosa hilo Jara alimfuata kwa karibu na kuingiza mkono wake katika makalio ya mshambuliaji huyo ambaye alihamaki kea hasira. Akihojiwa Tabarez amesema alimtetea Cavani akidai mwamuzi msaidizi alipaswa kuliona tukio hilo kwani ndiye aliyekuwa karibu zaidi kuliko mwamuzi wa kati. Hiyo sio mara ya kwanza kwa Jara kuwafanyia wachezaji wenzake uhuni pindi wanapokutana na timu hiyo kwani mwaka 2013 mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez alimpiga ngumi beki huyo baada ya kushinda uume wake wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment