KLABU ya Marseille imekubali ofa kutoka kwa West Ham United kwa ajili ya nyota wao wa kimataifa wa Ufaransa Dimitri Payet lakini wamemtaka mchezaji kuendelea kubakia hapo. Katika siku za karibuni mshambuliaji huyo alikutana na viongozi wa klabu hiyo kuzungumzia mustakabali wake na kumuhakikishia rais wa Marseille Vincente Labrune kuwa ataendelea kuitumikia timu hiyo. Hata hivyo, Payet sasa ameamua kuwa anataka kuondoka kufuatia fungu kubwa la pesa lililotolewa na West Ham. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao, klabu hiyo imedai kuwa makubaliano yalishafikiwa Juni na Payet pamoja na wakala wake kuwa mchezaji huyo ataheshimu mkataba wake mpaka utakapomalizika mwaka 2017. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa siku tatu zilizopita wakala wa mchezaji huyo aliomba mkutano mwingine na Labrune na baada ya kukutana alimtaarifu juu ya ofa hiyo kubwa ya euro milioni 30 waliyopata kutoka West Ham. Rais huyo alishtushwa na taarifa hizo na kwakuwa wakala huyo alikutana na West Ham bila kuwa taarifa ombi lake la kutaka mkataba wa mteja wake kuangaliwa upya lilikataliwa kwa kipindi ambacho wakala huyo alitaka.
No comments:
Post a Comment