Tuesday, June 30, 2015

MALDINI AITABIRIA MAKUBWA BARCELONA.

NGULI wa soka wa Italia, Paolo Maldini ametabiri kuwa Lionel Messi na wachezaji wa sasa wa Barcelona watakuja kuvunja rekodi zote. Katika msimu wake wa kwanza Camp Nou meneja Luis Enrique, Barcelona imefanikiwa kunyakuwa taji la La Liga, Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa ni mara ya pili katika historia klabu hiyo kunyakuwa mataji matatu mfululizo. Wakiwa wamefikia mafanikio waliyopata mwaka 2009 chini Pep Guardiola, Maldini anafikiri Messi, Neymar na Luis Suarez wanaweza kuisaidia Barcelona kuendelea kutengeneza historia zaidi katika kipindi kinachokuja. Maldini amesema Messi, Neymar na Suarez wameonyesha kiwango kikubwa msimu uliopita na anadhani wakiendelea hivyo wataiwwezesha klabu hiyo kuvunja rekodi zote zilizopo mbele yao.

No comments:

Post a Comment