RAIS wa zamani wa Barcelona, Joan Laporta amejinadi kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha analirejesha jina la UNICEF au shirika lolote la misaada ya kibinadamu katika fulana za timu hiyo kama akirejea tena madarakani katika uchaguzi wa mwezi ujao. Laporta ndiye aliyetengeneza dili la UNICEF miaka 10 iliyopita wakati akiwa rais kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 ambapo ilishuhudia nembo ya shirika hilo ikiwekwa katika fulana za timu hiyo kwa mara ya kwanza katika historia. Chini ya uongozi uliopita, ulioongozwa na Sandro Rosell na baadae Josep Maria Bartomeu umeshuhudia nembo ya wadhamini ya shirika la ndege la Qatar ikionekana mbele ya fulana huku nembo ya UNICEF ikiwekwa nyuma. Akijinadi katika kampeni za uchaguzi, Laporta amesema atafanya kila awealo kuhakikisha anatafuta wadhamini ambao wataweza kufanikisha hilo na kurejesha nembo ya UNICEF katika fulana za timu hiyo tena. Laporta anakabiliwa na upinnzani mkali kutoka kwa rais aliyepita Bartomeu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment