Tuesday, June 30, 2015

IVORY COAST YAKARIBIA KUPATA MRITHI WA RENARD.

SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast limetoa majina ya makocha watano waliopenya katika kinyang’anyiro cha kutafuta kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia kuondoka kwa Herve Renard. Maofisa wa shirikisho hilo wamesema vigezo vikubwa vinavyohitajika kwa kocha wanayemuhitaji ni uzoefu wa soka la Afrika na awe anazungumza kifaransa ili kumuwezesha kuwasiliana kirahisi sio tu na wachezaji wanaocheza soka nje bali hata wale waliopo ndani. Mojawapo ya majina yaliyotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Henyk Kasperczak (Pichani) ambaye amewahi kuinoa timu hiyo kati ya mwaka 1993 na 1994. Kocha huyo raia wa Poland mwenye umri wa miaka 68 pia amewahi kuzinoa timu za taifa za mali, Tunisia na Senegal. Wengine ni kocha wa zamani wa Guinea, Dr Congo na Mauritania Patrice Neveu, Michel Dusseyer ambaye naye amewahi kuinoa Guinea, Mreno Paulo Duarte na Frederic Antonetti akiwa kocha pekee ambaye hajawahi kufundisha soka Afrika. Ivory Coast imekuwa bila kocha toka alipoondoka Renard ambaye aliiwezesha nchi hiyo kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment