KLABU ya Manchester City imefanikiwa kumsajili mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19 Enes Unal kutoka klabu ya Bursaspor. Nyota huyo amefunga mabao manne katika mechi 35 za Ligi Kuu ya Uturuki alizoichezea timu hiyo lakini anaonekana atakuja kuwa moto baadae baada ya kuweka rekodi ya kufunga mabao 170 katika mechi 102 alizocheza katika timu za vijana. Kabla ya kuchagua kujiunga na City, Unal alikuwa akiwindwa pia na klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United. Rais wa Bursaspor, Recep Bolukbasi alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Unal anatarajiwa kwenda Uingereza mwishoni mwa wiki hii kukamilisha usajili huo.
No comments:
Post a Comment