Wednesday, June 24, 2015

NFF YARIDHISHWA NA UTETEZI WA KESHI.

SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF limesisitiza kuwa Stephen Keshi ataendelea kubakiwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na taarifa zinazomhusisha na kuomba kibarua katika timu ya Ivory Coast. Keshi aliorodheshwa miongoni mwa majina 60 ya makocha walioomba kibarua cha kuinoa nchi hiyo na Shirikisho la Soka la Ivory Coast. Taarifa hizo zilileta mkanganyiko na kufanya kamati ya nidhamu na sheria kukutana kwa dharura kujadili suala hilo huku Keshi mwenyewe akiitwa kujieleza na kukanusha taarifa hizo. Mwenyekiti wa kamati hiyo Christopher Green amebainisha kuwa uchunguzi zaidi utaendelea baada ya kusikiliza utetezi wa Keshi katika kikao chao kilichoketi jijini Abuja. Green aliendelea kudai kuwa wakati uchunguzi huo ukiendelea Keshi ataendelea na kibarua chake kama kawaida. Mbali na kuinoa Nigeria, Keshi pia amewahi kuzifundisha timu za taifa za Mali na Togo.

No comments:

Post a Comment