Monday, December 5, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: BOBAN ATIMULIWA KILI STARS.

KIUNGO Haruna Moshi-Boban ametimuliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars kutokana na sababu za utovu wa nidhamu alizozionyesha katika mchezo wa wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Zimbabwe wiki iliyopita. Akizungumza Dar es Salaam, Kocha wa Kilimanjaro Charles Mkwasa amesema kuwa wamemuondoa Boban katika kikosi hicho kutokana na kitendo chake cha kuondoka katika benchi ya wachezaji wa akiba kabla mchezo kumalizika ambapo timu hiyo ililala bao 2-0. Mkwasa amesema hakuna kocha yoyote anayeweza kuvumilia kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo hivyo wameona ni bora kumuondoa katika kikosi hicho ingawa alikiri kuwa kuondoka kwake kutaacha pengo katika kikosi hicho. Kocha aliendelea kusema kuwa kikosi chake hakikuanza vyema michuano hiyo kwa mwaka huu hivyo kwasasa anahitaji wachezaji wenye nidhamu na wanaojituma ili kufanikiwa kutetea taji hilo ambalo walilichukua mwaka jana.

No comments:

Post a Comment