Monday, December 5, 2011

MAS YANYAKUWA KOMBE LA SHIRIKISHO.

Kikosi kamili cha MAS
TIMU ya MAS ya Morocco jana ilifanikiwa kunyakuwa ushindi katika michuano Kombe la Shirikisho baada ya kuibanjua timu ya Africain ya Tunisia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida. Golikipa wa MAS Anas Zniti ndio alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuzuia mkwaju wa penati wa mchezaji Zied Ziadi kabla ya yeye mwenyewe kupiga penati ya mwisho na kuipa ushindi wa kwanza wa kihistoria timu yake hiyo. 
Anas Zniti, golikipa wa MAS
Ushindi huo umekuwa ni kama historia ikijirudia baada ya klabu nyingine kutoka Morocco ya FUS Rabat kuifunga Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo msimu uliopita. MAS ambaye ndio bingwa wa michuano hiyo imekunja kitita cha dola 660,000 ambapo mapema mwaka ujao watapambana na bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika timu ya Esperance katika kombe lililoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.

No comments:

Post a Comment