Monday, December 5, 2011

NAHODHA WA ZAMANI WA BRAZIL AFARIKI DUNIA.

MCHEZAJI soka wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil Socrates amefariki dunia akiwa na miaka 57. Nahodha huyo alijulikana zaidi mwaka 1982 wakati alipokiongoza kikosi cha Brazil katika michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huo kikosi ambacho kinasifika kwa kuonyesha kandanda safi kuliko kikosi chochote cha timu hiyo kilichopata kutokea. Lakini mbali na uchezaji soka mchezaji pia alikuwa akijulikana kwa unywaji wa pombe uliopitiliza kitu ambacho aliwahi kukiri kimemsababishia matatizo ya afya mpaka kupelekea kifo chake kilichotokea jana. Mbali na kuwa mcheza soka Socrates alikuwa na shahada ya udaktari aliohitimu akiwa na miaka 23 na pia alikuwa mwandishi na mchambuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo michezo pamoja na siasa na ameacha mke na watoto sita.

No comments:

Post a Comment