Monday, December 5, 2011

BLATTER APANIA KUISAFISHA FIFA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema Jumapili hii kuwa anataka kubadilisha taswira ya shirikisho hilo ambalo kwasasa limekumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo za rushwa. Blatter ambaye ni raia wa Switzerland alikataa mapema mwaka huu kwamba hana mpango wa kuachia ngazi kwani kuna mambo mengi ya kufanya ili kurudisha heshima ya shirikisho hilo ambayo inataka kutoweka. Kiongozi huyo wa FIFA ambaye hivi karibuni alijikuta katika vita nzito baada ya kauli yake kuhusiana na ubaguzi amesema yapo mambo ya kufanya ili kuhakikisha wanasafisha jina la FIFA. FIFA katika kipindi cha karibuni limekumbwa na matukio kadhaa ikiwemo lile la kuzipa nchi za Russia na Qatar uenyeji michuano ya kombe la Dunia 2018 na 2022 kuwa liligubikwa na rushwa huku tukio lingine likiwa la aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo Mohamed bin Hammam kufungiwa kufuatia kashfa ya kununua wapiga kura.

No comments:

Post a Comment