Monday, December 5, 2011

MAN UNITED KUIKWAA TENA CITY KATIKA FA CUP.

MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la Chama cha Soka cha Uingereza-FA Manchester City wamepangwa tena na mahasimu wao Manchester United katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo. City walifanikiwa kuwafunga United ambao ni mabingwa kihistoria wa michuano hiyo wakiwa wamenyakuwa kombe hilo mara 11 kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali msimu uliopita na kumaliza kiu yao ya miaka 35 bila kikombe. Katika ratiba ya michuano hiyo ambayo ilipangwa jana timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo zilipata bahati ya kucheza michezo yao katika hatua hiyo wakiwa nyumbani ambapo Arsenal itaikaribisha Leeds United katika Uwanja wa Emirates. Timu nyingine ni Chelsea itaikaribisha Portsmouth katika Uwanja wa Stanford Bridge huku Liverpool wakiwa wenyeji wa timu ya Oldham na Tottenham Hotspurs wakicheza na Cheltenham.

No comments:

Post a Comment