Thursday, December 15, 2011

TEVEZ ATAKA KUHAMIA BOCA JUNIORS.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Carlos Tevez amedai kuwa hahitaji kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza na anachotaka yeye ni kujiunga na klabu yake ya utotoni ya Boca Juniors. Tevez mwenye umri wa miaka 27 amekuwa nje ya mipango ya meneja wa City Roberto Mancini msimu huu na hajajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo toka akatae kuingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwezi Septemba. Timu za AC Milan, Paris Saint-Germain na Corinthians ya Brazil zimekuwa zikimnyemelea mshambuliaji huyo lakini mwenyewe amesema hana mpango wa kujiunga na klabu yoyote zaidi ya Boca Juniors. Tevez amesema kuwa hajali kama atakatwa mshahara wake na kwamba amechoka kusafiri mara kwa mara hivyo hatarudi tena Uingereza na anahitaji kuanza msimu na kucheza michuano ya Klabu Bingwa ya Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores akiwa na Boca Juniors.

No comments:

Post a Comment