Thursday, December 15, 2011

COLOMBIA YAMTIMUA KOCHA WAKE.

SHIRIKISHO la Soka la Colombia-FCF limesitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Lionel Alvarez. Taarifa ya FCF iliyotolewa na rais wake Luis Bedoya imefafanua kuwa wajumbe wa kamati ya shirikisho hilo hawakuwa na imani na kocha huyo kwamba ana uwezo wa kuiwezesha timu hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa wajumbe wa kamati hiyo wameamua kusitisha mkataba wa Alvarez na sasa wanahitaji kuchukua hatua za haraka ili kuziba pengo la kocha huyo ili timu hiyo iweze kushiriki vyema michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. Toka Alvarez achukue mikoba ya kukinoa kikosi hicho Septemba mwaka huu timu hiyo imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Bolivia, imetoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Venezuela na kufungwa na Argentina mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment