Thursday, December 15, 2011

BARCELONA YAIADHIBU AL SADD 4-0.

TIMU ya Barcelona imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Klabu bingwa ya Dunia baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Al Sadd ya Qatar kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika jijini Tokyo, Japan. Mabao mawili ya Barcelona yalifungwa na mchezaji Adriano katika dakika ya 25 akimalizia mpira baada ya kipa wa Al Sadd kushindwa kuondoa hatari langoni mwao huku la pili akifunga kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya 43 na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Seydou Keita dakika ya 64 akimalizia pasi murua iliyopigwa na Lionel Messi na bao la mwisho la Barcelona lilifungwa na Maxwell Cabelino dakika ya 81 na kuipeleka Barcelona fainali. Kilele cha michuano hiyo kitafikia Jumapili kwa mchezo wa fainali utakaozikutanisha timu za Barcelona na Santos ya Brazil mchezo ambao utafanyika jijini Yokohama, Japan

No comments:

Post a Comment