Wednesday, December 14, 2011
BECKENBAUER AUKANDIA MFUMO WA GOAL-LINE TECHNOLOGY.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer amesema hafurahishwi na utumiaji wa mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli. Kauli wa nyota huyo wa zamani imekuja kufuatia Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kudai kuwa mfumo huo umeonyesha mafanikio katika majaribio yake na unaweza kuanza kutumika katika Kombe la Dunia mwaka 2014 litalofanyika nchini Brazil. Beckenbauer mwenye umri wa miaka 66 hivi sasa amesema kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa kawaida wenye sheria nyepesi na unatakiwa ubaki hivyo. Mchezaji huyo wa zamani ambaye sasa ni rais wa klabu ya Bayern Munich amesema ni bora kutumika waamuzi wa nyongeza kuliko mfumo huo wa kompyuta. Beckenbauer ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia akiwa kama mchezaji na pia kama kocha amefafanua kuwa waamuzi wa ziada wanaweza kufanya kazi zaidi ya mfumo huo wa kompyuta ambao utakuwa ukifanya kazi moja tu kuangalia mpira kama umevuka goli wa la.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment