Wednesday, December 14, 2011

AS MONACO YANUNULIWA NA BILIONEA WA URUSI.

Rais wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa Etienne Franzi amedai kuwa klabu hiyo itamilikiwa na mfanyabiashara wa Urusi Dmitry Rybolovlev mwishoni mwa mwaka huu. Franzi amesema kila kitu kuhusu umilikishwaji wa klabu hiyo kitajulikana mwishoni mwa mwaka huu na kudai kuwa hizo ni habari njema kwa klabu hiyo na soka la Ufaransa kwa ujumla. Bilionea huyo ambaye kwa mujibu wa orodha ya mabilionea inayotolewa na gazeti maarufu la Forbes anashika namba 93 kwa utajiri duniani mwaka 2010 aliuza hisa zake kwa kampuni ya uzalishaji wa mbolea zinafikia kiasi cha dola bilioni 6.5. Monaco ambao ni mabingwa mara saba wa Ligi Kuu ya Ufaransa huku wakiwa wamefika hatua ya fainali katika michuano ya Klabu ya Bingwa ya Ulaya mwaka 2004 waliteremka daraja mwishoni mwa msimu uliopita na hivi sasa bado wanasuasua katika ligi daraja pili baada ya kucheza michezo 16 na kushinda mmoja tu.

No comments:

Post a Comment