Wednesday, December 14, 2011

ETO'O NA WENZIE KUFUNGIWA MECHI SABA NA FECAFOOT.

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Cameroon-Fecafoot huenda ikawafungia michezo saba wachezaji wake Samuel Eto’o, Eyong Enoh na Benoit Assou kwa makosa tofauti yanayowakabili. Eto’o na Enoh wao wanaweza kupewa adhabu hiyo kwa kuchochea mgomo katika kikosi cha timu ya taifa cha nchi hiyo wakati Assou yeye anaweza kufungiwa kwa kukataa mara kadhaa kukitumikia kikosi cha nchi yake. Kamati hiyo ilitarajiwa kufanya kikao chake Jumatatu jijini Younde ambacho kilihudhuriwa na Eto’o Makamu wa Rais wa Fecafoot Francis Mveng kocha wa kikosi hicho Denis Lavagne na msaidizi wake Ntoungou Mpile. Eyong hakuwepo wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo lakini aliwakilishwa na wakili wake huku Assou pamoja na barua waliyompa kuhudhuria kesi yake yeye hakuwepo kabisa na hakutuma mwakilishi yoyote.

No comments:

Post a Comment