Friday, December 9, 2011

VILLAS-BOAS AMNYEMELEA AYEW.

MENEJA wa timu ya Chelsea Andre Villas-Boas yuko katika harakati za kumnasa kiungo wa kimataifa wa Ghana Andre Ayew ambaye anaichezea klabu ya Marseille ya Ufaransa katika msimu ujao wa usajili. Meneja huyo raia wa Ureno kwasasa yuko katika mkakati mzito wa kukisuka kikosi cha Chelsea ambacho kimeonekana kusuasua msimu huu hivyo kuamua kuongeza damu changa nyingi katika msimu ujao. Mpango wa kocha huyo unatarajiwa kuanza kufanya kazi mapema katika kipindi cha dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Januari mwakani na moja ya dhamira yake ni kumsajili mshambuliaji huyo Marseille. Ayew mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akiwindwa pia na klabu ya Arsenal katika kipindi cha miezi ya karibuni lakini Chelsea wameonyesha nia ya dhati ya kumnyakuwa mchezaji huyo kwa kitita cha Euro milioni 10.

No comments:

Post a Comment