Friday, December 9, 2011

"MESSI NI BORA DUNIANI": NEYMAR.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil Neymar da Silva amekiri kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ndiye mchezaji bora duniani kwasasa. Kauli ya mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya Santos imekuja kufuatia nguli wa soka wa zamani wa nchi hiyo Pele kudai kuwa mchezaji huyo kinda anafuata nyendo zake na kwasasa ndiye mchezaji bora bora duniani ukimlinganisha na Messi. Neymar wakati akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kikosi chake kuwasili nchini Japani kwa ajili ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa la Dunia amesema ni heshima kubwa kwa gwiji huyo kumfananisha na yeye ingawa akakiri kuwa hadhani kama atafikia kiwango chake. Mchezaji huyo mwenye miaka 19 pia alipingana na kauli ya Pele aliyoitoa akidai kuwa Messi siyo bora kama alivyokuwa yeye kwa kufafanua kuwa yeye anadhani mshambuliaji huyo wa Barcelona ndiye bora duniani kwasasa.

No comments:

Post a Comment