Friday, December 9, 2011

MSENEGAL N'DOAYE AWA MCHEZAJI BORA DENMARK.

MCHEZAJI wa Kimataifa kutoka Senegal Dame N’Doye ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Denmark na Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Mshambuliaji mwenye miaka 26 anayekipiga katika klabu ya FC Copenhagen amekuwa katika kiwango bora msimu wa 2010-2011 baada ya kufunga mabao 25 katika michezo 31 aliyocheza na kuiwezesha timu yake kunyakuwa ubingwa tisa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo. Mchezaji huyo ambaye amezaliwa katika mji wa Thie ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Senegal alianza kucheza soka katika klabu ya nchini kwao ya Jeanne d’Arc kabla ya kuhamia Qatar kuichezea klabu ya Al-Saad mwaka 1996. Baadae alihamia klabu ya Academica de Coimbra ya Ureno na Panathinaikos ya Ugiriki kabla ya kujiunga na Copenhagen anayochezea`mpaka hivi sasa.

No comments:

Post a Comment