Friday, December 9, 2011

EL CLASICO: HAPATOSHI LA LIGA LEO.

Timu ya Real Madrid leo itawakaribisha mahasimu wao Barcelona katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Madrid ambao wanaongoza ligi hiyo kwasasa wakiwa na tofauti ya alama tatu nyuma ya Barcelona wataingia uwanjani huku wakiwa na kiu kubwa ya ushindi ili kuzidi kujizatiti kileleni na kuweka matumaini hai ya kunyakuwa ubingwa wa ligi hiyo ambao wameukosa kwa muda wa miaka mitatu sasa. Barcelona ambao msimu huu wamekuwa na rekodi isiyo ya kuridhisha katika michezo yao ya ugenini itakuwa na kibarua kigumu katika mchezo huo na Madrid ambayo wameonyesha kuwa katika kiwango bora msimu huu. Pamoja na rekodi hiyo Barcelona toka kuwasili meneja wake Pep Guardiola mwaka 2008 timu hiyo hiyo imekuwa mwiba mchungu kwa mahasimu wao Madrid kwa kuibuka kidedea katika michezo yao ilizozikutanisha timu hizo.

No comments:

Post a Comment