Sunday, December 11, 2011

GABON YATWAA TAJI LA VIJANA CHINI YA MIAKA 23.

TIMU ya taifa chini ya miaka 23 ya Gabon imeshinda taji lake la kwanza barani Afrika baada ya kufanikiwa kuifunga Morocco katika mchezo wa fainali ya michuano ya vijana ya umri huo uliofanyika jijini Marrakech, Morocco. Timu zote mbili zilishakata tiketi ya kucheza michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London hivyo mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya taji hilo la ubingwa wa vijana chini ya miaka 23. Misri nao walikata tiketi ya kucheza michuano ya Olimpiki baada ya kufanikiwa kuifunga Senegal kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mtoano wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo. Pamoja na kupoteza mchezo huo Senegal ambao wanashika nafasi ya nne watalazimika kucheza hatua ya mtoano na mshindi wanne wa michuano kama hiyo kutoka bara ya Asia ili waweze kufuzu michuano ya Olimpiki.

No comments:

Post a Comment