Tuesday, December 13, 2011

MTUKUTU DIOUF AWINDWA NA ANZHI MAKHACHKALA.

MSHINDI mara mbili wa tuzo za Mchezaji bora wa Afrika na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Senegal El Hadji Diouf ametajwa kama mmoja wa wachezaji wanaowindwa na klabu tajiri ya Anzhi Makhachkala. Diouf ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya daraja la kwanza nchini Uingereza ya Doncaster Rovers mkataba ambao utaisha Januari mwakani amesema mazungumzo kuhusu uhamisho wake yameshaanza ingawa hakuna makubaliano yoyote waliyofikia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema kuwa kucheza pamoja na Samuel Eto’o itakuwa ni heshima kubwa kwake lakini akasema kuwa hilo ni suala la kushauriana na familia yake kwanza kabla ya kufanya uamuzi wowote. Diouf ambaye alifungiwa kuichezea timu ya taifa ya Senegal kwa miaka mitano anaweza kupunguziwa adhabu hiyo baada ya kukubali kuhudhuria kesi yake itakayosikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Senegal amedai pia kuwindwa na klabu nyingine nchini Urusi pamoja na Los Angeles Galaxy.

No comments:

Post a Comment