Tuesday, December 13, 2011

IVORY COAST KUWEKA KAMBI DUBAI.

TIMU ya Taifa ya Ivory Coast inatarajiwa kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Dubai. Kikosi hicho ambacho kinajulikana kwa jina la utani la Tembo kimepania kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakuwa taji la michuano hiyo ambalo litakuwa la pili kwao, kitaelekea katika jiji hilo mwishoni mwa mwezi Desemba. Tembo hao wakiwa Dubai kwa ajili ya maandalizi kikosi hicho kinatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki na timu kubwa za taifa ingawa kocha wa timu hiyo Francois Zahoui hakutaja ni timu gani kwasababu taratibu za kutafuta timu hizo bado zinaendelea. Ivory Coast imepangwa kundi B katika michuano hiyo ikiwa na timu za Sudan, Burkina Faso na Angola ambapo katika mchezo wake wa kwanza itacheza na Sudan Januari 22 katika Uwanja wa Nuevo ulipo jijini Malabo nchini Equatorial Guinea.

No comments:

Post a Comment