NAHODHA wa timu ya Arsenal Robin Van Persie anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho katika ziara ya kimichezo nchini Nigeria mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo wanatarajiwa kufanya ziara nchini humo mwaka ujao ambapo mbali ya Van Persie pia watakuwa na nyota wao kama Theo Walcott, Alex Song, Gervinho, Thomas Vermaelen, Per Mertesacker, Mikel Arteta na Andre Arshavin.
Arsenal ilithibitisha ziara yake hiyo kupitia kwa Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Angus Kinnear kuwa timu hiyo itafanya ziara jijini Abuja baada ya kukagua na kuridhishwa na Uwanja wa Taifa uliopo katika mji huo mkuu. Kinnear ambaye alifunga safari hiyo akiwa na ofisa mwenzake Paul Johnson amesema amefurahishwa na mapokezi aliyopata na anaamini kuwa nyota wake watapata mapokezi kama hayo ambapo pia alifurahishwa na idadi ya mashabiki wa klabu aliyoiona ambayo inakadiriwa kufikia milioni mbili.
No comments:
Post a Comment