Tuesday, December 13, 2011

CELTIC YATOZWA FAINI KWA USHANGILIAJI HARAMU.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limeitoza klabu ya Celtic faini ya Euro 15,000 kufuatia ushangiliaji haramu uliofanywa na mashabiki wa timu hiyo mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi ya Ulaya dhidi ya Rennes. Klabu hiyo ilithibitisha kupokea barua ya faini ikiwa haina maelezo mengine ambapo wamesema kwasasa wanajipanga kuangalia kama walipe faini hiyo au wakate rufani kupunguziwa adhabu hiyo. Jopo la maofisa wa Kamati ya Nidhamu ya UEFA ilifikia maamuzi hayo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mapolisi waliokuwa wakisimamia mchezo huo uliochezwa Novemba 3. Tabia hiyo ya ushangiliaji uliokatazwa wa mashabiki wa Celtic umeonekana kuwa sugu ambapo mapema mwezi huu timu hiyo iliepuka kupewa adhabu kwa matatizo kama hayo katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Scotland ambao uliisha kwa sare ya bila ya kufungana dhidi ya timu ya Hibernian.

No comments:

Post a Comment