Tuesday, December 13, 2011

ARSENAL KUKOSA HUDUMA YA SANTOS MWA MIEZI 3.

BEKI wa Arsenal Andre Santos anatarajiwa kukaa nje uwanja kwa muda wa miezi mitatu kwasababu ya kuumia kifundo cha mguu. Santos anayecheza kama beki wa kushoto alipata majeraha hayo wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Olympiakos uliochezwa nchini Ugiriki ambapo Arsenal walipoteza mchezo huo na sasa beki huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji nchini Brazil baadae wiki hii. Katika taarifa iliyotolewa katika tovuti ya klabu hiyo imethibitisha kuwa ni kweli mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki hii na atakuwa nje ya uwanja katika kipindi kinachokadiriwa kuwa cha miezi tatu ambapo kila mmoja katika klabu hiyo anamtakia mchezaji huyo kupona haraka. Santos mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na klabu hiyo mwezi Agosti mwaka huu akiwa ameichezea timu hiyo michezo 14 na kufunga mabao mawili.

No comments:

Post a Comment