Monday, December 19, 2011

ETO'O AGOMA KUKATA RUFANI KUPINGA ADHABU YAKE.

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o amesema hatarajii kukata rufani juu ya adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot la kumfungia kucheza mechi 15 za timu hiyo. Mwanasheria wa Eto’o Barrister Gabriel ambaye pia anamwakilisha mchezaji mwenzie Eyong Enoh katika kesi hiyo ya Kamati ya Nidhamu ya Fecafoot amesema kwa niaba ya mteja wake kuwa alipewa maelekezo na Eto’o kuwa asikate rufani juu ya adhabu hiyo aliyopewa. Gabriel aliendelea kusema kuwa Fecafoot walitakiwa wafikirie kwanza kabla ya kutoa adhabu hiyo kwani haikuwa na maana yoyote kumpa adhabu kubwa kama hiyo wakati mchezaji mwenyewe alikuwa akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake. Kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Eto’o alitishia kumshitaki Makamu wa Rais wa Fecafoot Francis Mveng na pia alipokea kauli zisizo za kiungwana kutoka kwa viongozi wa shirikisho hilo ambapo toka aongoze mgomo huo amekuwa na maelewano yasio mazuri.

No comments:

Post a Comment