Monday, December 19, 2011

RAIS WA SEVILLA KWENDA JELA MIAKA SABA.

RAIS wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido amehukumiwa miaka saba na nusu jela kufuatia kukutwa na hatia ya makosa ya rushwa katika mahakama ya Malaga nchini Hispania. Kesi hiyo ambayo haihusiana na klabu Sevilla imemkumba Del Nido akiwa kama mshauri wa kisheria wa Baraza katika mji wa Marbela akiwa na wenzake 16 katika kesi hiyo. Del Nido mweye miaka 54 aliteuliwa kushika wadhifa huo wa kuwa mshauri wa kisheria wa baraza hilo na aliyekuwa Rais wa klabu Atletico Madrid ambaye pia alikuwa meya wa mji wa Marbella. Del Nido ameiongoza klabu ya Sevilla kwa mafanikio toka mwaka 2002 ambapo amefanikiwa kushinda Kombe la Uefa mwaka 2006 na 2007, kombe la mfalme mwaka 2007 na 2010 pamoja na kuwa washiriki wa michuano ya Ligi ya Ulaya katika kipindi chote cha uongozi wake.

No comments:

Post a Comment